WIZARA YA AFYA NA
USTAWI WA JAMII
Kwa kushirikiana na
TAASISI YA BENJAMIN WILLIAM MKAPA HIV/AIDS
TANGAZO LA KAZI (LA MARUDIO)
Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwa kushirikiana na Taasisi ya
Benjamin William Mkapa HIV/AIDS inatekeleza Mradi wa kuimarisha mifumo ya
huduma za afya ( Health Systems Strengthening) kupitia ufadhili wa Mfuko wa
Dunia wa kupambana na UKIMWI, Kifua Kikuu na Malaria - Mzunguko wa 9 ( Global
Fund Round 9). Baadhi ya malengo ya mradi ni pamoja na; kuongeza wataalam wa
afya, ili kuimarisha huduma za UKIMWI, Kifua Kikuu, Malaria na huduma
nyinginezo katika Halmashauri za Wilaya zenye upungufu wa watumishi wa afya.
Katika kipindi cha miaka minne ( 2011 -
2014) ya utekelezaji wa mradi huu, Taasisi imefanikiwa kuajiri watumishi wa
afya 452 na wakufunzi wa afya 182 na kuwapangia kazi katika Halmashauri za
Wilaya 70 na Vyuo vya afya 43.
Ili kuhakikisha malengo ya Mradi huu
yanafikiwa, Taasisi inazo nafasi zilizo wazi kama zinavyoanishwa hapo chini:
a)Nafasi za kazi katika Halmashauri za
Wilaya:
Kada/
Wilaya
|
Afisa Tabibu (Clincial Officer)
|
Daktari (Medical Officer)
|
Muuguzi
( Nurse)
|
Fundi Sanifu Maabara ( Lab
Technologist)
|
Fundi Sanifu Madawa (Pharmaceutical
Technologist)
|
Nafasi Wazi (Vacant Post)
|
1.Chunya DC
|
1
|
|
|
|
|
1
|
2. Kigoma Vijijini
|
1
|
|
|
|
|
1
|
3. Mufindi DC
|
|
|
1
|
|
|
1
|
4. Mkinga DC
|
|
1
|
|
|
|
1
|
5. Njombe DC
|
|
|
|
1
|
|
1
|
6. Ukerewe DC
|
3
|
|
|
|
|
3
|
7. Kibondo DC
|
|
|
|
|
1
|
1
|
Jumla
|
5
|
1
|
1
|
1
|
1
|
9
|
b)Nafasi za wakufunzi katika Vyuo vya
Afya:
Chuo
|
Kada
|
Nafasi wazi
|
Chuo cha Uuguzi na Ukunga Mkomaindo - Mtwara
|
Afisa Muuguzi ( Nursing Officer)
|
2
|
Chuo cha Uuuguzi na Ukunga Korogwe - Tanga
|
Afisa Muuguzi ( Nursing Officer)
|
2
|
Chuo cha Uuguzi na Ukunga Newala - Mtwara
|
Afisa Muuguzi ( Nursing Officer)
|
1
|
Chuo cha Uuguzi na Ukunga Tanga
|
Afisa Muuguzi ( Nursing Officer)
|
3
|
Chuo cha Uuguzi na Ukunga Bagamoyo - Pwani
|
Afisa Muuguzi ( Nursing Officer)
|
2
|
Chuo cha Maafisa Tabibu Kigoma
|
Daktari (Medical Officer)
|
4
|
Chuo cha Maafisa Tabibu Kilosa - Morogoro
|
Daktari (Medical Officer)
|
1
|
Chuo cha Maafisa Tabibu Mafinga - Iringa
|
Daktari (Medical Officer)
|
2
|
Chuo cha Maafisa Tabibu Musoma - Mara
|
Daktari (Medical Officer)
|
3
|
Chuo cha Maafisa Tabibu Sumbawanga - Rukwa
|
Daktari (Medical Officer)
|
5
|
Chuo cha Maafisa Tabibu Wasaidizi Maswa - Shinyanga
|
Daktari (Medical Officer)
|
5
|
Jumla
|
|
30
|
Izingatiwe kwamba:
·
Ajira ndani ya mradi huu itatolewa kwa mkataba wa si zaidi ya
miezi kumi na mbili (12) na mara baada ya kukamilika kipindi hiki, waajiriwa
wote katika mradi huu watatakiwa kujiunga katika utumishi wa
umma kulingana na taratibu na kanuni za ajira za Serikali.
·
Mradi hautapokea maombi ya wataalam waliopo katika ajira za
utumishi wa umma au katika Taasisi/Vyuo vya mashirika ya dini (FBOs) na
wataalam wenye umri zaidi ya miaka 45.
·
Mishahara itatolewa kulingana na sifa na ujuzi wa mtumishi husika
pamoja na maslahi mengineyo yaliyobainishwa katika mradi.
Maombi yote
yaambatanishwe na:
1.
Barua ya maombi ya kazi, ikipendekeza Halmashauri za Wilaya 2 na
Vyuo vya afya Viwili mwombaji anavyopendelea kupangwa kikazi, na pia aonyeshe
ridhaa ya kujiunga na utumishi wa umma, baada ya
kukamilika kwa mkataba.
2.
Nakala ya cheti cha Taaluma na cheti cha kidato cha 4 pamoja na
cha 6 (iwapo anacho), na viwe vimethibitishwa na Hakimu au Wakili.
3.
Nakala ya cheti cha usajili/leseni, cheti cha mazoezi kwa vitendo
(internship) kwa kada zinazohusika kama vile; madaktari, wafamasia,
wateknolojia na wauguzi
4.
Picha mbili (2) – saizi ya Pasipoti na maelezo binafsi (CV),
ikionyesha umri, anuani kamili ya Posta na barua pepe na namba ya simu ya
kiganjani, pamoja na anuani/ namba ya kiganjani ya wadhamini wako wasiopungua
watatu (3).
Mwisho wa kupokea maombi haya ni tarehe
18 Novemba 2014
Maombi yote yatumwe
kwa njia ya Posta kwa anuani ifuatayo:
Afisa Mtendaji Mkuu,
Taasisi ya Benjamin Mkapa HIV/AIDS Foundation, S.L.P. 76274, DAR ES SALAAM.
Show Konversi KodeHide Konversi Kode Show EmoticonHide Emoticon