BENJAMIN WILLIAM MKAPA FOUNDATION JOBS - NOV 2014


WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII
 Kwa kushirikiana na
 TAASISI YA BENJAMIN WILLIAM MKAPA HIV/AIDS
 TANGAZO LA KAZI (LA MARUDIO)
 Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwa kushirikiana na Taasisi ya Benjamin William Mkapa HIV/AIDS inatekeleza Mradi wa kuimarisha mifumo ya huduma za afya ( Health Systems Strengthening) kupitia ufadhili wa Mfuko wa Dunia wa kupambana na UKIMWI, Kifua Kikuu na Malaria - Mzunguko wa 9 ( Global Fund Round 9). Baadhi ya malengo ya mradi ni pamoja na; kuongeza wataalam wa afya, ili kuimarisha huduma za UKIMWI, Kifua Kikuu, Malaria na huduma nyinginezo katika Halmashauri za Wilaya zenye upungufu wa watumishi wa afya.
Katika kipindi cha miaka minne ( 2011 - 2014) ya utekelezaji wa mradi huu, Taasisi imefanikiwa kuajiri watumishi wa afya 452 na wakufunzi wa afya 182 na kuwapangia kazi katika Halmashauri za Wilaya 70 na Vyuo vya afya 43.
Ili kuhakikisha malengo ya Mradi huu yanafikiwa, Taasisi inazo nafasi zilizo wazi kama zinavyoanishwa hapo chini:
a)Nafasi za kazi katika Halmashauri za Wilaya:
Kada/
Wilaya
Afisa Tabibu (Clincial Officer)
Daktari (Medical Officer)
Muuguzi
( Nurse)
Fundi Sanifu Maabara ( Lab Technologist)
Fundi Sanifu Madawa (Pharmaceutical Technologist)
Nafasi Wazi (Vacant Post)
1.Chunya DC
1
1
2. Kigoma Vijijini
1
1
3. Mufindi DC
1
4. Mkinga DC
1
5. Njombe DC
1
1
6. Ukerewe DC
3
3
7. Kibondo DC
1
1
Jumla
5
1
1
1
1
9
b)Nafasi za wakufunzi katika Vyuo vya Afya:
Chuo
Kada
Nafasi wazi
Chuo cha Uuguzi na Ukunga Mkomaindo - Mtwara
Afisa Muuguzi ( Nursing Officer)
2
Chuo cha Uuuguzi na Ukunga Korogwe - Tanga
Afisa Muuguzi ( Nursing Officer)
2
Chuo cha Uuguzi na Ukunga Newala - Mtwara
Afisa Muuguzi ( Nursing Officer)
1
Chuo cha Uuguzi na Ukunga Tanga
Afisa Muuguzi ( Nursing Officer)
3
Chuo cha Uuguzi na Ukunga Bagamoyo - Pwani
Afisa Muuguzi ( Nursing Officer)
2
Chuo cha Maafisa Tabibu Kigoma
Daktari (Medical Officer)
4
Chuo cha Maafisa Tabibu Kilosa - Morogoro
Daktari (Medical Officer)
1
Chuo cha Maafisa Tabibu Mafinga - Iringa
Daktari (Medical Officer)
2
Chuo cha Maafisa Tabibu Musoma - Mara
Daktari (Medical Officer)
3
Chuo cha Maafisa Tabibu Sumbawanga - Rukwa
Daktari (Medical Officer)
5
Chuo cha Maafisa Tabibu Wasaidizi Maswa - Shinyanga
Daktari (Medical Officer)
5
Jumla
30
Izingatiwe kwamba:
·         Ajira ndani ya mradi huu itatolewa kwa mkataba wa si zaidi ya miezi kumi na mbili (12) na mara baada ya kukamilika kipindi hiki, waajiriwa wote katika mradi huu watatakiwa kujiunga katika utumishi wa umma kulingana na taratibu na kanuni za ajira za Serikali.
·         Mradi hautapokea maombi ya wataalam waliopo katika ajira za utumishi wa umma au katika Taasisi/Vyuo vya mashirika ya dini (FBOs) na wataalam wenye umri zaidi ya miaka 45.
·         Mishahara itatolewa kulingana na sifa na ujuzi wa mtumishi husika pamoja na maslahi mengineyo yaliyobainishwa katika mradi.
Maombi yote yaambatanishwe na:
1.     Barua ya maombi ya kazi, ikipendekeza Halmashauri za Wilaya 2 na Vyuo vya afya Viwili mwombaji anavyopendelea kupangwa kikazi, na pia aonyeshe       ridhaa ya kujiunga na utumishi wa umma, baada ya kukamilika kwa mkataba.
2.     Nakala ya cheti cha Taaluma na cheti cha kidato cha 4 pamoja na cha 6 (iwapo anacho), na viwe vimethibitishwa na Hakimu au Wakili.
3.     Nakala ya cheti cha usajili/leseni, cheti cha mazoezi kwa vitendo (internship) kwa kada zinazohusika kama vile; madaktari, wafamasia, wateknolojia na wauguzi
4.     Picha mbili (2) – saizi ya Pasipoti na maelezo binafsi (CV), ikionyesha umri, anuani kamili ya Posta na barua pepe na namba ya simu ya kiganjani, pamoja na anuani/ namba ya kiganjani ya wadhamini wako wasiopungua watatu (3).
Mwisho wa kupokea maombi haya ni tarehe 18 Novemba 2014
Maombi yote yatumwe kwa njia ya Posta kwa anuani ifuatayo:
Afisa Mtendaji Mkuu, Taasisi ya Benjamin Mkapa HIV/AIDS Foundation, S.L.P. 76274, DAR ES SALAAM.
Majibu yatatolewa kwa watakaofanikiwa tu ifikapo tarehe 28 Novemba 2014

Previous
Next Post »
Thanks for your comment

Don't Forget To Join US Our Community
×